Fonetiki

  DIBAJI

Katika mada hii tutajadili maana ya fonetikipamoja na  matawi ya fonetiki.

FONETIKI

Ni tawi la isimu ambalo linachunguza na kufafanua sauti za lugha ya mwanaadamu. kwa kawaida fonetiki huchunguza sauti zote za lugha ya kusemwa na binanaadamu.



MATAWI YA FONETIKI

kuna matawi tofauti ya fonetiki, nayo ni;
  1. Fonetiki matamshi
  2. Fonetiki akustiki
  3. Fonetiki masikizi
  4. Fonetiki tiba matamshi
Katika mada yetu hii tutazungumzia tawi moja la fonetiki ambalo ni fonetiki Matamshi.


Fonetiki matamshi
   ni tawi la fonetiki ambalo huchunguza au inashughulikia matamshi ambayo mwanaadamu anayotoa. Fonetiki  matamshi hususan huchunguza sauti za lugha ya mwanaadamu.Tawi hili hubainisha sauti za lugha kwa kuchunguza harakati  za ala sauti zinazo husika. kwa vile fonetiki matamshi huchunguza ala sauti za lugha kwa hivyo tunajadili ala sauti mbalimbali za tugha ya mwanaadamu.
  Aala sauti za lugha
Ala sauti ni viungo vya mwili vya mwanaadamu vinavyotumika kumuweza binaadamu kutowa sauti.
  Mchoro ufuatao tnaonesha ala sauti za lugha ya mwanaadamu.




katika mchoro huu tunaona kuwa kuna ala sauti ambazo ni ala tuli na sogezi.
Ala tuli ni zile zinazotulia wakati wa utamkaji wa vitamkwa, (zisizotinga). Na ala sogezi ni zile zinazojisogeza sogeza wakati wa kuzitamka (zinazotinga).
 Tuangalie video zifuatazo ili tujifunze zaidi.








kwa hivyo, hapa ndio mwisho wa uwasilishaji wetu.
  

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

UTUNGAJI