UTUNGAJI
Katika somo hili tutaangalia vipengele vifuatavyo, Maana ya utungaji Makusudio ya kutoa matangazo Mambo ya kuzingatia wakayi ya kutoa tangozo Sehem kuu za tangazo MAANA YA TANGAZO Tangazo ni habari fupi inayosomwa kwa mdomo au iliyoandikwa kwa lengo la kuwafikishia walengwa ujumbe Fulani. Matangazo hutokea kayika magazeti, redio, television, mabango, kuta za nyumba na kadhalika. MAKUSUDIO YA KUTOA MATANGAZO Kwa ajili ya kutoa taarifa kam vile taarifa za mikutano na sherehe Kuudha bidhaa au kutoa huduma. Matangazo yanayohusu utoaji wa taarifa ni kama vile matangazo ya mukutano, vikao vya harusi, warsha, makongamano, mialiko kwenye nyumba za ibada na kadhalika. Matangazo yanayohusu kuuza bidhaa au huduma ni kama vile matangazo yahusuyo zabuni, usafiri wa ndege na kadhalika. MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA TANGAZO Tangazo liandikwe kwa namna inayojenga shauku ya kupata kile kinachotangazwa Tangazo liandikwe kwa namna inayovutia macho Tangazo liandikwe kwa namna ya kumfan...